WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Sunday 7 May 2017

Njia 7 za Kuondokana na Hofu ya Mafanikio

Tumia njia hizo ili kuondokana na hofu ambayo imejengeka ndani mwako kwani hofu ni adui namba moja wa maisha yako ya mafanikio kama utaendelea kuibeba.

1. Muombe  mwenyezi Mungu.
Kila wakati na  kila siku hakikisha unamuomba Mwenyezi Mungu akusaidie kuweza kuondokana na hofu kubwa ambayo imekuwa ikijengeka ndani yako. Haijalishi ni imani gani uliyonayo ila hakikisha unamuomba Mungu akusaidie juu ya hilo.

2. Acha kujilinganisha na wengine.
Mafanikio ni haki yako, kila wakati hivyo kama unaamini juu ya hili, unachotakiwa kufanya ni kuweza kusimama wewe kama wewe katila jambo lako ulifanyalo, watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu tunataka kujifananinisha na wengine. Na athari kubwa ambayo ambayo itatokea pale unapotaka kujifananisha na wengine ni kwamba utajiona huwezi kufanikiwa.
Nb; hivyo wewe ni mwenye mafaniko kuanzia sasa, endapo utaacha mara moja kujilinganisha na wengine.

3. Chukua hatua ya kuendelea mbele kivitendo.
Tumia njia hii katika kusonga mbele, acha maneno weka vitend. Watu wengi tumejenga maneno mbele kuliko vitendo na hii hofu kubwa imejengeka sana miongoni mwa watu, hivyo ukijijengea uwezo wa kivitendo zaidi utakufanya uondakane na hofu iliyopo ndani yako.

Inawezekana kabisa labda ukawa tayari umeshanza kufanya vitu fulani ila huna imani ya kufanikiwa zaidi, ninachoweza kukwambia ni kwamba, siri ya mafanikio yako inatokana na vile ambavyo unaamini, hivyo kuanzia sasa anza kuwaza chanya dhidi ya kile ukifanyacho, kwani kama endapo ukiamini, utaenda kufanya jambo hilo kwa nguvu na bidii na kuleta matokeo chanya.

4. Acha kuangalia tatizo kama tatizo, bali tafuta majibu ya tatizo husika.
Moja ya matatizo/ changamoto ambazo zinatokea katika jamii ni chanzo kikubwa cha kuleta hofu ya mafanikio. Kwa mfano mtu anafanya biashara fulani ila baada ya muda fulani kuna changamoto inajitokeza katika biashara hiyo, utashangaa muda fulani mtu uyo anaacha kufanya jambo hilo nakufanya jingine.

Hivyo ili kuishinda hofu iliyomo ndani yako unachotakiwa kufanya, ni kuhakikisha kila changamoto inayojitokeza ni sehemu mafanikio na sio sehemu ya kushindwa.
Kwani kuna mwandishi fulani, aliwahi sema " fear is danger, success is real.

5. Baki na mawazo chanya kila wakati.
Mara nyingi hofu  zimekuwa zikitawala katika mioyo na fikra zetu, hii ni kutokana na mawazo hasi tuliyoyabeba, kwa mfano watu wengi wanaamini ya kwamba wao kufaulu katika mtihani wa kutoka hali ya umaskini ni suala gumu sana.

Lakini ukweli n kwamba kama kweli unataka kufanikiwa katika jambo ambalo unataka kulifanya hakikisha ya kwamba unawaza chanya juu ya jambo, kwani kuna usemi usemao uwazo mtu ndivyo atakavyokuwa, hivyo anza kuwaza chanya kwa kila jambo kuanzia sasa, kwani kufanya hivyo ni njia tosha ya ulekeo wa mafanikio yako.

6. Anza na kidogo ulichonacho.
Njia moja wapo ya kuendelea kusonga mbele na kuagana na woga ni ile hali ya kuanza na kile ulinaonacho, kwani aliyenacho huongezewa. Usisubiri mpaka ufikishe kiasi fulani cha fedha ndo uanze jambo hilo, kwani haba na haba hujaza kibaba na ngoja ngoja yaumiza matumbo.

mpaka ufikishe kiasi fulani ndo uanzishe jambo lako, ila jambo la msingi ni kuhakikisha kwa kile kidogo ulichonacho kumbuka kuanza kukifanyia kazi huku ni nidhamu ya muda na fedha ikipita mkondo wake.


7. Fanya kitu unachokiogopa.
Haua ya sita ni kwamba, njia bora ya kuondokana na hofu ni kufanya kile kitu ambacho unakiogopa. Kwa mfano kama ulikuwa unaogopa kufanya biashara fulani anza kufanya sasa, kama ulikuwa unaogopa kuonesha kipaji chako anza sasa. Usitake kuendelea kuangalia nani atasema nini bali simama wewe kama wewe huku, ukisonga mbele kila wakati.

No comments:

Post a Comment