WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Friday 4 March 2016

Ban na wasiwasi na kuenea misimamo mikali Afrika

Na Renalda Mwarabu
 
 Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Ban Ki Moon akitoa wasiwasi wake juu kuhusu mashambulizi ya kigaidi barani Afrika
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya makundi ya kigaidi huko Burkina Faso, magharibi mwa Afrika na kuitaka dunia isimame kukabiliana na hatari ya kuenea misimamo mikali barani Afrika.
Ban Ki moon amesema hayo huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso na kuongeza kuwa, nchi za ukanda huo zinapaswa kushrikiana kukabiliana na matatizo mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa kazi, ubaguzi na kinga ya kutoshitakiwa baadhi ya watu.
Ban alianza ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Afrika siku ya Jumatano kwa kuanzia nchini Burkina Faso ambako alilakiwa na Alpha Barry, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.
Jana Alkhamisi alionana na Rais Roch Marc Christian Kaboré wa nchi hiyo, kama ambavyo alitembelea pia kituo kimoja na kuwasaidia chakula watoto wadogo na kituo kimoja cha watoto wenye maradhi ya Ukimwi.
Mbali na Burkina Faso, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepangiwa kutembelea pia nchi za Mauritania na Algeria.
Ziara ya Ban Ki moon inafanyika katika hali ambayo hivi karibuni kulitokea mashambulio ya kigaidi katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou na kupelekea kuuawa zaidi ya watu 30. Chanzo Radio Terhan

No comments:

Post a Comment