Mataifa tajiri duniani ya G7 yamekataa ombi la Uingereza la kutaka vikwazo kuwekwa dhidi ya Urusi baada ya shambulizi baya la kemikali linaloaminiwa kuendeshwa na mshirika wa Urusi, Syria.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi alisema kuwa kundi la G7 halikuwa na nia ya kuisukuma Urusi kuenda kwa ukuta na badaa yake lilitaka kuwepo mazungumzo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, kwa sasa anafunga safari kutoka nchini Italia kwa mazungzo mjini Moscow.
Amesema kuwa rasi wa Syria hawezi kushirii katika mchakato kuhusu hatma ya nchi.
Siku ya Jumanne bwana Putin aliutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchuzi huru kuhusu shambulizi la kemikali, katika mji unaodhibitiwa na waasikwenye mji wa Khan Sheikhoun lililowaua watu 89.
Alisema pia kuwa amesikia kuwa mashambulizi bandia yanafanywa ili kuiwekea lawana serikali ya Syria.
Syria ilikana kufanya shambulizi hilo, lakini Marekani ilijibu kwa kufyatua makombora kuenda kwa kambi ya wanahewa nchini Syria.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Italia Angelino Alfano, ambaye aliandaa mkutano wa G7 katika mji wa Lucca, alisema kuwa mawaziri hao walitaka kuzungumza a na Urusi kuitaka imushinikize rais wa Syria Bashar al-Assad baadla ya kuisukuma Urusi hadi kwa ukuta
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
|
|
No comments:
Post a Comment