WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Sunday 16 April 2017

TCRA Yatoa Somo kwa Wanafunzi Vyuoni

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini na wananchi kutumia huduma za mawasiliano kwa faida, badala ya kuzitumia kujiburudisha pekee.
Mhandisi wa Masafa wa TCRA, Francis Mihayo alisema hayo hivi karibuni wakati wa kongamano la vyuo vikuu kujadili matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha. Mihayo alisema kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao baadhi wameingia matatani kutokana na kuTOzingatia sheria.
Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, John Semindu alisema wameamua kuandaa kongamano hilo ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kujifunza matumizi sahihi ya na kujiepusha kusambaza ujumbe wenye lengo la kusababisha uvunjifu wa sheria. 

Semindu alisema kutokana na kukua kwa huduma za mawasiliano nchini na duniani, ni watu wachache wanaotumia huduma hizo zaidi ya kuwasiliana.
“Tunatakiwa twende mbali zaidi ya kuwasiliana na kutumiana ujumbe kutufanya tucheke, bali tunaweza kutumia huduma za Tehama kujiajiri na kuajiri wengine ni eneo muhimu katika kurahisisha kazi na kuchochea ubunifu ambao ndiyo msingi wa maendeleo,” alisema Semindu.
Richard Gwele, kutoka Taasisi ya Smart Education na Mwangaza Jafar ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, walisema elimu zaidi inapaswa kutolewa ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi hasa kwenye mitandao ya jamii.
Gwele alisema iwapo wanafunzi watatumia mitandao vizuri itawasaidia kupata kujisomea mambo mbalimbali hasa yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia duniani.
Alisema wanafunzi hawajatumia hata nusu ya mitandao katika kujielimisha, hivyo wanatakiwa kubadilika.

No comments:

Post a Comment