WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Sunday 7 May 2017

Simba yarejea Kileleni VPL, Mchezo wake na African Lyon ulikuwa hivi...

SIMBA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo uliotokana na mabao ya Ibrahim Hajib na beki wa Lyon, Hamad waziri aliyejifunga, unawafanya Wekundu wa Msimbazi wafikishe pointi 62 baada ya kucheza mechi 28 wakiwarudisha nafasi ya pili, mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 59 za mechi 26.  

Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Ludovic Charles wa Tabora aliyesaidiwa na Robert Luhemeja wa Mwanza na Vincent Mlabu wa Morogoro, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.

Mshambuliaji Ibrahim Hajib alitangulia kuifungia Simba kwa shuti la mbali lililombabatiza beki wa Lyon, Hassan Isihaka na kutinga nyavuni dakika ya 37 baada ya kupokea pasi ya kiungo Muzamil Yassin. 

Hata hivyo, bao hilo lilidumu kwa dakika nane tu, kabla ya kiungo wa Lyon, Omar Abdallah kuisawazishia timu yake kwa shuti la mbali pia lililowapita mabeki wa Simba na kipa wao, Mghana, Daniel Agyei.

Kipindi cha pili Simba wakakianza vizuri tena na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 54  kufuatia bekki wake, Hamad Waziri kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa kichwa wa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo. 

Baada ya bao hilo, Simba walianza kucheza kwa kujihami zaidi kuulinda ushindi wao, huku Lyon wakipambana kutafuta bao la kusawazisha bila mafanikio. 

No comments:

Post a Comment