Rais John Magufuli jana alitumia staili nyingine ya kumshtaki kwa wananchi mbunge wa Ubungo, Said Kubenea katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Chuo hicho kipo katika jimbo hilo linaloongozwa na mbunge huyo wa Chadema na hivyo katika hali ya kawaida alitakiwa kuhudhuria sherehe hizo za ufunguzi, lakini Rais Magufuli alipomuulizia ili azungumze chochote kwa niaba ya wananchi wake, hakuwapo.
Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kutumia staili hiyo kumchongea mbunge baada ya kufanya hivyo mapema mwezi Machi alipokuwa Kilwa mkoani Lindi.
Siku hiyo, akiwa njiani kwenda mikoa ya kusini kwa ziara ya kikazi, Rais alimtaka mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), Vedasto Ngombale Mwiru kutoa ahadi ya kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kutoka kwenye fedha za mfuko wa jimbo, lakini mbunge huyo aligoma akitoa utetezi kuwa hana fungu hilo.
Jitihada za Rais kumshawishi atoe ahadi hiyo hazikufanikiwa baada ya mbunge huyo kusema hataweza kufanya hivyo kwa sababu fedha za mwaka huu zimekwisha akisisitiza, “msemakweli ni mpenzi wa Mungu.”
Ndipo Rais alipowaambia wananchi kuwa wamemsikia mbunge wao na baadaye kutoa ahadi yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
|
|
No comments:
Post a Comment