Na Renalda Mwarabu
Jumuiya mbalimbali zisizo za serikali (NGO's) zimetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya wanakijiji huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Innocent Segihobe ambaye ni Katibu Mkuu wa jumuiya zisizo za serikali
amesema uchunguzi huo unapaswa kuweka wazi majukumu ya kufanya baada ya
mauaji ya wanakijiji cha Nyanzale katika eneo la Rusthuru huko Kivu
Kaskazini, Congo DR. Segihobe amewatuhumu viongozi wa kisiasa wa eneo la
Rusthuru kwamba wanahusika katika kudumisha machafuko na mapigano huko
Kivu Kaskazini.
Mapigano yaliyotokea baina ya wakimbizi na wakazi wa kijiji cha Rusthuru yalianza baada ya kupatikana maiti ya mkimbizi mmoja katika eneo hilo. Wakimbizi hao wanawatuhumu wanakijiji kuwa ndio waliomuua mkimbizi mwenzao.
Watu watano wameripotiwa kuuawa na nyumba zaidi ya 40 kuteketezwa kwa moto katika machafuko hayo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Rusthuru wamekimbilia katika kambi za askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.Chanzo radio Terhan

No comments:
Post a Comment