WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Showing posts with label Home. Show all posts
Showing posts with label Home. Show all posts

Tuesday, 23 February 2016

MUHULA MPYA WA MASOMO WATANGAZWA CHUONI HABARI MAALUM

NA ELIA GUMBO

Muhula mpya wa masomo ya uandishi wa habari pamoja na masomo ya Uongozi na Utawala umetangazwa kuanza rasmi tarehe 9 mwezi wa tatu mwaka wa masomo 2016 katika chuo cha Habari Maalum kilichopo eneo la Ngaramtoni jijini Arusha.
Sehemu ya eneo la mazingira na Jengo la madarasa katika Chuo cha Habari kilichopo Arusha Tanzania. Picha na Neema Dandida

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha masomo ya Uandishi wa Habari, mwalimu Nehemia Rubondo ,alipokutana na wanahabari wa Hmc broadcasting na kusema kuwa,ni wakati muafaka kwa wale wenye ndoto za kuwa waandishi wa habari mahiri pamoja na viongozi wenye sifa stahiki kujiunga na muhula mpya wa masomo unaotaka kuanza.

Mkuu wa kitengo cha masomo ya Uandishi wa Habari na mawasiliano Bwana Nehemia Rubondo akiwa katika moja ya darasa akifundisha .Picha na Esther Dominic

Mwalimu Rubondo amesema ,wale wote wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa ngazi ya cheti, wanatakiwa kuwa na ufaulu wa  D  nne kwa masomo ya kidato cha nne au cheti cha veta chenye sifa stahiki huku wale watakaotaka kujiunga kwa ngazi ya stashahada wawe na matokeo ya ufaulu wa D moja na S moja kwa masomo ya kidato cha sita au wenye cheti cha masomo husika.

Akieleza maono ya chuo hicho Rubondo amesema ,wamekuwa na mkakati wa kuwaandaa watendaji wenye taaluma ya kutosha iliyojengwa juu ya ufundishwaji kwa vitendo ili kuleta mabadiliko ya mtu binafsi ,jamii inayomzunguka ,Taifa na duniani kote kwa msingi mzuri wa kimaadili.


Tuesday, 16 February 2016

NI MSIMU MWINGINE KUTUPELEKA KATIKA KUPATA KATIBA MPYA

Na: Elia Simon Gumbo

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema mchakato wa Kura ya Maoni ya Katiba mpya umeanza baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
 
Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja wakati wadau wa siasa nchini wakimtaka Rais Dk. John Magufuli, kutoendelea na Kura ya maoni badala yake mchakato wa Katiba mpya urudi nyuma baadhi ya mambo yaliyo kwenye Katiba iliyopendekezwa yarekebishwe.
 
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva .
Itakumbukwa kuwa mchakato wa Katiba mpya uliingia dosari baada ya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupinga mfumo wa Serikali Tatu uliokuwa umependekezwa na Tume ya Jaji mstaafu Joseph Warioba, iliyokusanya maoni nchi nzima na matokeo yake kuzaa kundi lililojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
 
“Tulikuwa tunangoja tumalize uchaguzi, kama vile ambavyo Mnyamwezi anavyobeba mzigo, unamaliza mmoja unakwenda kwa mwingine. Sasa tumemaliza (uchaguzi mkuu), tunakwenda kwa lingine (Kura ya Maoni),” alisema Jaji Lubuva.
 
Aliongeza: “Tunaliangalia na kama Tume tutakuja kuwajulisha wananchi hali ikoje, tuliahirisha (Kura ya Maoni) ili tumalize hili (uchaguzi mkuu).” alisema Jaji Lubuva na kuongeza.
 
“Hili ni suala linalohitaji mambo ya bajeti kubwa na ndiyo tumetoka kwenye uchaguzi na serikali ndiyo inaanza, kwa hiyo ni suala ambalo tunaliangalia na baadaye wananchi watajulishwa,” alisema Jaji mstaafu Lubuva.
 
Alipoulizwa kuhusu makadirio ya bajeti ya kuendesha kura hiyo ya maoni, Lubuva alisema: “Hilo niulize siku nyingine, sina zaidi ya hapo kwa leo.”
 
Rais Magufuli alipokuwa akihutubia Bunge la 11 siku ya kulizindua Novemba 20, mwaka jana, alisema serikali yake imepokea kiporo cha mchakato wa Katiba ambao haukukamilika katika awamu iliyomtangulia kutokana na kutokukamilika kwa wakati kwa uandikishaji wapiga kura. 
 
“Napenda kuwahakikishia kuwa tunatambua na kuthamini kazi kubwa ya kizalendo iliyofanywa na wananchi walioshiriki hatua ya awali ya ukusanyaji wa maoni kuhusu Katiba mpya, Tume ya Marekebisho ya Katiba na Bunge la Katiba lililotupatia Katiba Inayopendekezwa. Tutatekeleza wajibu wetu kama ulivyoainishwa katika Sheria ya Marekebisho ya Katiba,” alisema Rais Magufuli.  
 
Mbali na muundo wa serikali tatu, baadhi ya mambo ambayo Ukawa walitaka yawe kwenye Katiba mpya ni mamlaka ya Rais kupunguzwa, ushindi wa Rais uwe zaidi ya asilimia 50, Tume huru ya Uchaguzi, matokeo ya Rais kupingwa mahakamani, kuwe na mgombea binafsi, mawaziri wasitokane na wabunge, na muundo mpya wa Bunge la Muungano.
 
Oktoba 2, 2014, Bunge Maalum la Katiba chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Samuel Sitta, lilipitisha Katiba inayopendekezwa na kuiwasilisha kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Oktoba 8, ili mchakato wa Kura ya Maoni uendelee.
 
Kutokana na kutoka Bungeni kwa wajumbe wa bunge hilo kutoka kundi la Ukawa, kulikuwa na hofu kwamba akidi haitotimia na hivyo Katiba haitapita.
 
Baada ya kura kupigwa, aliyekuwa Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk. Thomas Kashililah, alisema idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar wakiwamo wa Ukawa waliosusa ambao kura zao zilihesabiwa kuwa ni `Hapana'  jumla yao ni 219.
 
Kwa mujibu wa idadi hiyo, theluthi mbili ya kura hizo kutoka Zanzibar ambazo ndiyo zilizokuwa zikihofiwa zaidi kufanya uamuzi, zilipaswa kuwa 146.
 
Akitangaza matokeo hayo, Dk. Kashililah alisema katika kura za wazi kutoka Zanzibar katika kila ibara, kura za juu kwa ibara moja zilikuwa 109 huku kura za chini zikiwa 106, ambazo hazikutosha kutimiza masharti ya theluthi mbili.
 
Kura za wazi za `Hapana' kwa mujibu wa Dk. Kashililah, kura za juu zilizokataa ni nane huku za chini kukataa ibara za Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, zikiwa kura tano.
 
Katika mchanganuo wa kura hizo, kura za siri ndizo zilizookoa jahazi, ambapo ibara iliyopigiwa kura chache zaidi za siri za `Ndiyo' ilipata kura 38 na ibara zilizopata kura za juu zilipata kura 39.
 
Kura za siri za `Hapana' zikiwa kura moja moja na katika ibara chache mno. Baada ya kutangaza matokeo ya kura hizo za wazi na za siri kwa upande wa `Hapana' na `Ndiyo,' ibara zote za Rasimu ya Katiba zilipata kura za chini za 146 na kadirio la juu la kura 148 na kuibua shangwe kubwa, kabla hata ya kura kutoka Tanzania Bara kutangazwa.
 
Kwa upande wa Tanzania Bara kulikuwa na wajumbe  411 wakiwamo wa Ukawa, wajumbe 335 walipiga kura. 
 
Kwa mujibu wa Dk. Kashililah, kila ibara ilipata wastani wa kura 331 mpaka 334, na hivyo kuzidi theluthi mbili iliyokuwa ikihitajika ya 274.

MAFUNZO KWA VITENDO YANAVYOKIPATIA SIFA CHUO CHA HABARI MAALUM.

Chuo cha Habari Maalum kinachotoa mafunzo ya Uandishi wa Habari pamoja na Uongozi na Usimamizi kilichopo Jijini Arusha kimejizolea umaarufu katika ukanda huu wa kaskazini kwa utoaji wake wa mafunzo ulioegemea zaidi katika vitendo.
  Kutokana na sifa hiyo, Chuo hicho kimeweza kupata tuzo mbalimbali ikiwamo ile ya utoaji elimu bora kwa ukanda huu wa kaskazini katika maonyesho ya nane nane Mwaka 2015.
 Chuo hiki kimekuwa kikitoa mafunzo katika ngazi ya Shahada na Stashahada na kimekuwa kikipokea pia wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi.
Na Diu Mwiko
Wanafunzi wa ngazi ya Stashada katika fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano wakiwa na mwalimu wao Bwana Zephania Kikumbo(Aliyevaa shati la blue)wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kurekodi Muziki(Picha na Nickson Mafuru)                                



Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Congo anaekwenda kwa jina la Solomono Mdogo akirekodi wimbo wake katika studio za Chuo Cha Habari Maalum,wakati wanafunzi hao wakifanya mazoezi kwa vitendo.(Picha na Nicksoni Mafuru)



Renalda Mwarabu Mwanafunzi wa Stashahada katika fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano akiwa studio katika kusoma kwa vitendo.(Picha na Nickson Mafuru)



Mazezi kwa Vitendo ni miongoni mwa sifa ambazo vyuo vingi nchini havina kutokana na uhaba wa vifaa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi,hali hiyo ni tofauti na chuo cha Habari Maalum ambapo kuna vifaa vya kutosha na mazingira rafiki kwa kujifunzia.

SEMINA YA SELF AWARENESS YAKUTANISHA VIJANA MBALIMBALI KATIKA CHUO CHA HABARI MAALUM

  Vijana kutoka vyuo mbalimbali Jijini Arusha wamekutana katika Semina ilikuwa na ujumbe wa Self awereness is more than money iliyotelewa na Mjasiriamali Bi Gracy Lyimo Pamoja na Ndugu Maxwell Chaila ambaye alifundisha kuhusu   Self Employment  can take your life into first class,Semina hiyo ilifanyika katika viunga vya Chuo cha Habari Maalum Jijini Arusha Mapema wiki iliyopita.

Na Diu Mwiko

Bi Gracy Lyimo akielezea kuhusu jinsi gani mtu anaweza akajitambua  mwenyewe..(Picha Na Nickson Mafuru)

Aidha katika Semina hiyo Bi Gracy amewataka vijana hao kujitambua pamoja na kutambua malengo yao na kuyafanyia kazi.

Nae msemaji wa pili katika semina hiyo Ndugu Maxwell Chaila aliongelea suala la kujiajiri mwenyewe na kusema kuwa linaweza kukuweka katika daraja la juu(Self employment can take your life into first class).

Katika semina hiyo Ndugu Maxwell amewataka vijana kufikiria kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa hali ambayo itawafanya kuwa huru.

Ndugu Maxwell Chaila mmiliki wa kampuni ya Ulinzi Jijini Arusha akifafanu kuhusu mambo matatu ambayo ni muhimu ili mtu aweze kujiajiri mwenyewe ambayo ni kujenga nidhamu,malengo pamoja na kujiunga na wajasiriamali.(Picha na Nickson Mafuru)















Akiwakaribisha wasemaji hao mkuu wa Chuo cha Habari Maalum Bwana Jackson Kaluzi amesema kuwa semina kama hizo ni jambo la msingi sana kwani linaenda sambamba na maono ya Chuo hicho kitu ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi pindi watakapo hitimu masomo yao.

Mkuu wa Chuo cha Habari Maalum Bwana Jackson Kaluzi wa kwanza kulia akifuatilia kwa makini Semina hiyo,wa pili kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Ndugu Lazorus Laiser,na wa tatu ni Ndugu Nestory Ihano Mkuu wa kitengo cha Uongozi na Utawala na pia ni mlezi wa wanafunzi chuoni hapo.(Picha na Nickson Mafuru).














Mwalimu Jastine Peter kutoka chuo  cha Habari Maalum aliyefanikisha kufanyika kwa semina hiyo akishirikiana na serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Habari Maalum pamoja na Chuo Kikuu Cha Mount Meru akitoa shukrani kwa wageni .(Picha Na Nickson Mafuru)
Burudani pia hazikukosekana ,mmoja wa wanafunzi kutoka katika chuo cha Habari Maalum anaekwenda kwa jina la Depper akionesha kipaji chake cha kuimba wakati wa semina hiyo(Picha Na Nickson Mafuru)


Baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya semina hiyo.(Picha na Nickson Mafuru)