DAR ES SALAAM: Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, Ridhiwani Kikwete amefunguka kuwa, kuna watu wanamchonganisha baba yake na utawala uliopo madarakani wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’.
Mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuliibuka maneno yaliyotengenezwa na ukurasa au akaunti yenye jina la Jakaya Mrisho Kikwete Fanpage yakioneshwa kuwa ni ya Rais JK, yaliyokuwa yakikosoa utawala uliopo madarakani kuwa unatumika vibaya dhidi ya kundi la wasio nacho (si busara kuyachapisha neno kwa neno).
Akitolea ufafanuzi jambo hilo, Ridhiwani alilithibitishia Risasi Mchanganyiko kuwa maneno hayo siyo ya baba yake na kwamba wanaofanya hivyo wana lengo la kumgombanisha mzazi wake huyo na utawala uliopo madarakani. “Sina hakika, lakini nadhani hao ni watu wanaolenga kugombanisha utawala.
“Nimeona hiyo page (ukurasa) inayozunguka mitandaoni na nimeguswa kueleza ukweli juu ya hilo. “Ukurasa huo siyo ukurasa rasmi wa mashabiki wa Jakaya Kikwete (baba yake) wala siyo ukurasa wake. Hakuna sehemu aliyowahi kuandika wala kusema maneno hayo.
“Naomba kutoa angalizo kwa wanaofanya matumizi mabaya ya mitandao kuwa watakuja kuingia matatizoni kwa kutumia majina ya watu kuchafua au kugombanisha watu.
“Kwa wale waliokwazwa na ujinga huo, kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete, tunawaomba radhi sana. Jitihada zimeanza kuwabaini wanaofanya hivyo. Tuendelee kusaidia maendeleo ya nchi.
Umoja wetu ndiyo maendeleo yetu,” alimalizia Ridhiwani ili kuweka sawa jambo hilo ambalo liliibua gumzo kwa baadhi ya watu walioamini kuwa ni maneno ya kiongozi huyo mstaafu na kwamba aliulenga utawala uliopo madarakani.
Mara kadhaa kumekuwa na watu wanaotumia vibaya majina ya watu likiwemo la JK kufungua kurasa au akaunti feki kisha kuandika maneno au kuweka sauti zenye nia ovu, jambo ambalo hulenga kuwachafua wahusika hivyo mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya wanaobainika kufanya hivyo ili kukomesha uhuni huo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
|
|
No comments:
Post a Comment