WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Tuesday, 11 April 2017

Serengeti Boys kucheza mechi ya kirafiki na Gabon


Dar es Salaam.Timu ya Taifa ya Vijana 'Serengeti Boys' iliyoko kambini nchini Morocco wiki ijayo itacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Gabon.

Serengeti Boys inajiandaa kushiriki fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika mwezi ujao nchini Gabon.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema  mchezo huo utachezwa baada ya Gabon kuomba mechi hiyo.

"Hii ni nafasi nyingine kwetu. Wenzetu (Gabon) walituomba na mchezo huo utachezwa siku yoyote wiki ijayo. Tuna bahati jwa kuwa Gabin pia wabashiriki fainali  na kocha anasema ni mchezo muhimu kwa kikosi chake,"alisema Lucas.

Lucas aliongeza kuwa mchezo huo utachezwa nchini Morocco.

Serengeti imeshacheza na Ghana na pia inatarajia kucheza na Cameroon baadye mwezi huu na hivyo itakuwa imecheza na timu tatu zinazoshiriki fainali hizo.

Tanzania imepangwa Kundi B na timu za Niger, Angola na mabingwa watetezi Mali na itaanza kutupa karata yake Mei 15 kwa kuchuana na Mali.                  


No comments:

Post a Comment