WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Saturday 20 February 2016

RATIBA MPYA MAZOEZI YA UANDAAJI VIPINDI YATAKIWA CHUONI HABARI MAALUM.



NA Elia Simon Gumbo

Mlezi wa wanafunzi  katika chuo cha habari maalum Bwana Nestory Ihano amehimiza  uongozi wa chuo hicho kuwasilisha  rasmi ratiba ya mazoezi kwa vitendo ambayo yamekuwa yakiwasaidia wanafunzi kupata uzoefu  wa kazi wanazosomea katika kipindi cha muhula mpya wa mwaka 2016 .

Bwana Ihano akielezea umuhimu wa ratiba hiyo ya  mazoezi ya urushaji vipindi amesema itasaidia wanafunzi masomo ya Uongozi na Uandishi wa Habari kuweza  kuutumia muda wao wa kimasomo vizuri kwa kujipatia ujuzi utakaoleta mafanikio ya maisha yao ya chuoni  na baadae katika maeneo ya kazi.

Naye makamu mkuu wa taaluma wa chuo cha Habari maalum bwana Lazarus Laizer ameeleza kuwa kuchelewa kidogo kwa ratiba hiyo kumetokana na mabadiliko ya maboresho ya mtaala wa masomo , mabadiliko ya kiuongozi pamoja na maboresho ya vifaa.
Makamu mkuu wa Taaluma chuo cha Habari Maalum  Bwana Lazarus Laizer  wakati alihojiwa na mwandishi wa Hmc  broadcasting kutolea ufafanuzi suala la  ratiba ya mazoezi ya urushaji vipindi chuoni hapo. Picha na Joshua Bimila

Bwana Laizer amesema wataleta mfumo mpya utakaowawezesha wanafunzi kuchagua aina ya vipindi wanavyotaka kuviandaa  ili kuleta ufanisi katika maeneo yote ya mafunzo ikiwemo  upande wa magazeti ,redio na televisheni.

Naye waziri wa elimu katika serikali ya wanafunzi ya chuo cha Habari maalum  ndugu Albin Michavao,amethibitisha kupata taarifa hizo za maboresho ya kitaaluma  na kuwataka wanafunzi wawe tayari kufanya kazi kwa  ushirikiano na bidii kwani ndio msingi wa mafanikio .

Mmoja wa wanafunzi wa habari maalum Winifrida nicolaus  ameeleza kufurahishwa na mpango huo wa kuendelea kwa  mazoezi hayo kwani yamekuwa yakiwandaa wanafunzi kupata ujuzi na kuwaongezea uwezo wa kujiamini wakiwa chuoni na hata nje ya chuo katika utendaji wa kazi mbalimbali.



No comments:

Post a Comment