WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Tuesday 23 February 2016

MUHULA MPYA WA MASOMO WATANGAZWA CHUONI HABARI MAALUM

NA ELIA GUMBO

Muhula mpya wa masomo ya uandishi wa habari pamoja na masomo ya Uongozi na Utawala umetangazwa kuanza rasmi tarehe 9 mwezi wa tatu mwaka wa masomo 2016 katika chuo cha Habari Maalum kilichopo eneo la Ngaramtoni jijini Arusha.
Sehemu ya eneo la mazingira na Jengo la madarasa katika Chuo cha Habari kilichopo Arusha Tanzania. Picha na Neema Dandida

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha masomo ya Uandishi wa Habari, mwalimu Nehemia Rubondo ,alipokutana na wanahabari wa Hmc broadcasting na kusema kuwa,ni wakati muafaka kwa wale wenye ndoto za kuwa waandishi wa habari mahiri pamoja na viongozi wenye sifa stahiki kujiunga na muhula mpya wa masomo unaotaka kuanza.

Mkuu wa kitengo cha masomo ya Uandishi wa Habari na mawasiliano Bwana Nehemia Rubondo akiwa katika moja ya darasa akifundisha .Picha na Esther Dominic

Mwalimu Rubondo amesema ,wale wote wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa ngazi ya cheti, wanatakiwa kuwa na ufaulu wa  D  nne kwa masomo ya kidato cha nne au cheti cha veta chenye sifa stahiki huku wale watakaotaka kujiunga kwa ngazi ya stashahada wawe na matokeo ya ufaulu wa D moja na S moja kwa masomo ya kidato cha sita au wenye cheti cha masomo husika.

Akieleza maono ya chuo hicho Rubondo amesema ,wamekuwa na mkakati wa kuwaandaa watendaji wenye taaluma ya kutosha iliyojengwa juu ya ufundishwaji kwa vitendo ili kuleta mabadiliko ya mtu binafsi ,jamii inayomzunguka ,Taifa na duniani kote kwa msingi mzuri wa kimaadili.


2 comments:

  1. Wanufaika wa kozi hizi changamkieni fursa hii, chuo hiki ni bora kusini mwa jangwa la Sahara kwa kozi ngazi ya cheti na stashahada

    ReplyDelete