WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Thursday 25 February 2016

SAFARI YA UJENZI CHUONI HABARI MAALUM YAENDELEA VIZURI



Na Renalda Mwarabu
Mkuu wa chuo bwana Jackson Kaluzi akizungumzia maendeleo ya ujenzi (picha na Renalda Mwarabu).
Wakati ujenzi wa studio na maktaba ukiendelea chuoni Habari Maalum, Mkuu wa chuo bwana Jackson Kaluzi amesema tangu ujenzi ulipoanza mpaka sasa wanaamini kuwa ujenzi utakamilika ndani ya miezi sita kama walivyo panga kwani hadi sasa maendeleo ni mazuri.

Kaluzi amesema imani yao ni kubwa hasa juu ya mkandarasi anayesimamia ujenzi huo kwani anaonyesha juhudi katika utendaji wake, ambapo kila wiki na kila mwezi kuna hatua zinazotakiwa kufikiwa  na matarajio yao yanaonekana kukamilika.
 
Eneo ambalo ujenzi unaendelea Chuoni Habari Maalum ( Picha na Renalda)
Aidha amesema pamoja na kuwepo na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kufikisha vifaa vya ujenzi katika eneo la ujenzi lakini hayo yote yameshughulikiwa.

Kwa upande wake Injinia wa Elerai Constraction Company Limited ni muda mfupi tangu waanze takribani mwezi mmoja lakini hadi sasa wamefika hatua ya juu zaidi ya muda walioutumia.
 
Injinia Elitosha Kimaro akizungumzia mwenendo wa ujenzi(Picha na Renalda)
Bwana Kimaro amezitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja naukosekanaji wa maji maeneo ya karibu na kazi, hivyo hivyo inawagalimu kufuata maji mbali, pia ardhi ina vumbi ambayo ni changamoto katika kazi, lakini wanajitahidi kudhibiti kwa kumwaga maji mengi ardhini.

Injinia huyo amemaliza kwa kusema kuwa, kazi hii imekuwa na faida kubwa kwa wakazi wanaoishi kuzuguka chuo cha Habari Maalum, kwani wameweza kupata ajira.

No comments:

Post a Comment