WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Thursday 25 February 2016

HITILAFU YAJITOKEZA CHUONI HABARI MAALUM NA KUSABABISHA HALI YA SINTOFAHAMU KWA WANAFUNZI




Na Renalda Mwarabu
                                Darasa lililopatwa na mfumuko wa vigae (Picha na Renalda Mwarabu).
Hitilafu imetokea Katika  chumba cha darasa kilichoko ghorofani chenye namba LR 07, katika chuo cha Habari Maalum  kilichopo Ngaramtoni Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha mara baada ya kutokea mfumuko wa vigae sakafuni nakusababisha hali ya sintofahamu kwa wanafunzi.


Hali hiyo imetokea wakati mwalimu na wanafunzi wakiwepo darasani n tayari kwa kuanza masomo pindi ambapo mmoja wa wanafunzi wa darasa hilo ambaye pia ni waziri wa elimu chuoni Habari Maalum alipokuwa akimsaidia mwalimu kuaandaa mashine ya ufundishaji (projekta).

 
Mwanafunzi Albin Michavo akizungumzia  namna ambavyo hitilafu ilivyotokea (Picha na Renalda Mwarabu).
Waziri huyo wa elimu Bwana Albin Michavo amesema hali ya sintofahamu ililikumba darasa na kusababisha wanafunzi kukimbia huku wakitoka nje ya darasa na kuacha vitu vyao.


Akitoa mtazamo wake amesema hali hiyo imetokea kwasababu vigae vimeonekana kuwa vimebananishwa na kukosa nafasi , hivyo ni rahisi sana hali hii kujirudia mara kwa mara.


Amesema si mara ya kwanza kutokea kwa hali hii, kwani hata muhula uliopita hitirafu kama hii ilikwisha wahi kutokea  katika darasa walilowahi kutumia lenye namba ya 09 na kuwapelekea kuhama darasa.


Kwa upande wake mwalimu alikuwa akifundisha katika darasa hilo, ambaye pia ni mwalimu kutoka uingereza, mwalimu Christopher Singh amesema chumba hicho si salama sasa kwa shughuli za masomo, hivyo imewabidi kuhamia chumba chenye namba LR 05, kwa ajili ya kuendelea na masomo.


Ikumbukwe kuwa mwaka uliopita hitirafu kama hii imewahi kutokea mara kwa mara, si katika madarasa tuu lakini pia katika koldo .


Wanafunzi waliopatwa na janga hilo ni kutoka darasa la stashahada ya kwanza A na B kwani walikuwa wamechangamana.


Lakini mpaka sasa bado haijajulikana ni nini kilichosababisha hitirafu hiyo.

No comments:

Post a Comment