WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Friday, 4 March 2016

TAZAMA VIDEO HII KUHUSU NIDHAMU

Mwandaaji ni
Renalda na Jane Mafupa

Museveni asema hatogawana madaraka na wapinzani


Na Renalda Mwarabu
 

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema hawezi kugawana madaraka na kambi ya upinzani kwani alishinda kihalali kwenye uchaguzi mkuu wa Februari 18.

Akizungumza na kiongozi wa chama cha upinzani cha Farmers Party of Uganda (FPU), Meja Jenerali Benon Biraaro, Rais Museveni amesema anakaribisha pendekezo la kufanya mazungumzo na wapinzani kwa ajili ya kujadili mustakabali wa kisiasa wa taifa lakini hawezi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayowashirikisha wanasiasa wa upinzani.

Amesema uchaguzi ulikuwa fursa nzuri kwa wanasiasa kujitafutia vyeo na kama wapinzani walishindwa kuwashawishi wapiga kura, wanapaswa kusubiri hadi uchaguzi ujao na wala si kutumia njia za mkato kuingia serikalini.

Huku hayo yakijiri kuna tetesi kwamba kiongozi wa upinznai, Kizza Besigye ametoweka na hajulikani aliko. Duru za habari zinasema Besigye ambaye alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani hayuko tena nyumbani kwake. Polisi ya Uganda imekataa kuthibitisha au kukanusha suala hilo.( Chanzo Radio Terhan)

Serikali yavipongeza Vyombo vya Habari kwa kuhabarisha jamii vyema

Na Renalda Mwarabu
 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Habari akivishukuru vyombo vya habari kwa kuhabarisha watanzania kipindi cha uchaguzi na pia katika siku mia za kwanza za Rais wa awamu ya tano na Mhe.John Pombe Magufuli na kuwapongeza kwa kuonyesha weledi na ukomavu katika uandishi wa Habari.
 
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kuwahabarisha watanzania vyema katika mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na katika kipindi cha siku mia za kwanza za awamu ya tano ya utawala wa Mheshimiwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli.
Naibu Waziri uyo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wadau wa Habari katika tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited.
“Hakika mmeonesha uwezo mkubwa, weledi na ukomavu mkubwa wa kisiasa na uzalendo kwa nchi yetu”.Alisema Bi.Wambura.
Mhe.Wambura pia alieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ina dhamira ya dhati kabisa ya kushirikiana na wadau wote vikiwemo Vyombo vya Habari, ambapo pia mchakato wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambao ulishasomwa kwa mara ya kwanza bungeni bado Serikali inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali juu ya namna bora ya kuboresha Muswada huo.
Naibu Waziri uyo alikazia umuhimu wa upashaji habari na kusema ni jambo muhimu sana katika nchi yetu na kwaiyo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo iko tayari kufanya kazi na wadau wote.
“Kama Serikali hatuwezi kuwakwepa wadau na ndio maana hata utaratibu wetu wa kushughulikia makosa kwenye Vyombo vya Habari umebadilika. Tumekuwa ni walezi zaidi badala ya kuwa viranja. Tunashauriana zaidi kuliko kutoa adhabu. Tunaelimisha zaidi kuliko kusubiliana”
Naibu Waziri uyo pia ameupongeza uongozi mpya wa jukwaa la wahariri na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa karibu katika kutatua masuala mbalimbali ya Habari.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Magazeti ya Mwananchi Bw.Francis Nanai ameipongeza serikali kwa kuweka jitihada zaidi katika kuboresha mahusiano mazuri na vyombo vya Habari na pia kwa afrika mashariki Tanzania iko katika nafasi nzuri ukilinganisha na wenzetu katika suala la uhuru wa vyombo vya habari.
(Chanzo Mo bog)

Ban na wasiwasi na kuenea misimamo mikali Afrika

Na Renalda Mwarabu
 
 Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Ban Ki Moon akitoa wasiwasi wake juu kuhusu mashambulizi ya kigaidi barani Afrika
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya makundi ya kigaidi huko Burkina Faso, magharibi mwa Afrika na kuitaka dunia isimame kukabiliana na hatari ya kuenea misimamo mikali barani Afrika.
Ban Ki moon amesema hayo huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso na kuongeza kuwa, nchi za ukanda huo zinapaswa kushrikiana kukabiliana na matatizo mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa kazi, ubaguzi na kinga ya kutoshitakiwa baadhi ya watu.
Ban alianza ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Afrika siku ya Jumatano kwa kuanzia nchini Burkina Faso ambako alilakiwa na Alpha Barry, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.
Jana Alkhamisi alionana na Rais Roch Marc Christian Kaboré wa nchi hiyo, kama ambavyo alitembelea pia kituo kimoja na kuwasaidia chakula watoto wadogo na kituo kimoja cha watoto wenye maradhi ya Ukimwi.
Mbali na Burkina Faso, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepangiwa kutembelea pia nchi za Mauritania na Algeria.
Ziara ya Ban Ki moon inafanyika katika hali ambayo hivi karibuni kulitokea mashambulio ya kigaidi katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou na kupelekea kuuawa zaidi ya watu 30. Chanzo Radio Terhan