Na Renalda Mwarabu
Darasa lililopatwa na mfumuko wa vigae (Picha na Renalda Mwarabu).
Hitilafu imetokea Katika
chumba cha darasa kilichoko ghorofani chenye namba LR 07, katika chuo
cha Habari Maalum kilichopo Ngaramtoni
Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha mara baada ya kutokea mfumuko wa vigae
sakafuni nakusababisha hali ya sintofahamu kwa wanafunzi.
Hali hiyo imetokea wakati mwalimu na wanafunzi wakiwepo
darasani n tayari kwa kuanza masomo pindi ambapo mmoja wa wanafunzi wa darasa
hilo ambaye pia ni waziri wa elimu chuoni Habari Maalum alipokuwa akimsaidia
mwalimu kuaandaa mashine ya ufundishaji (projekta).
Mwanafunzi Albin Michavo akizungumzia namna ambavyo hitilafu ilivyotokea (Picha na Renalda Mwarabu). |
Waziri huyo wa elimu Bwana Albin Michavo amesema hali ya
sintofahamu ililikumba darasa na kusababisha wanafunzi kukimbia huku wakitoka
nje ya darasa na kuacha vitu vyao.
Akitoa mtazamo wake amesema hali hiyo imetokea kwasababu
vigae vimeonekana kuwa vimebananishwa na kukosa nafasi , hivyo ni rahisi sana
hali hii kujirudia mara kwa mara.
Amesema si mara ya kwanza kutokea kwa hali hii, kwani hata
muhula uliopita hitirafu kama hii ilikwisha wahi kutokea katika darasa walilowahi kutumia lenye namba
ya 09 na kuwapelekea kuhama darasa.
Kwa upande wake mwalimu alikuwa akifundisha katika darasa
hilo, ambaye pia ni mwalimu kutoka uingereza, mwalimu Christopher Singh amesema
chumba hicho si salama sasa kwa shughuli za masomo, hivyo imewabidi kuhamia
chumba chenye namba LR 05, kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Ikumbukwe kuwa mwaka uliopita hitirafu kama hii imewahi
kutokea mara kwa mara, si katika madarasa tuu lakini pia katika koldo .
Wanafunzi waliopatwa na janga hilo ni kutoka darasa la
stashahada ya kwanza A na B kwani walikuwa wamechangamana.
Lakini mpaka sasa bado haijajulikana ni nini
kilichosababisha hitirafu hiyo.
No comments:
Post a Comment