Na Renalda Mwarabu
Mkuu wa chuo bwana Jackson Kaluzi akizungumzia maendeleo ya ujenzi (picha na Renalda Mwarabu). |
Wakati ujenzi wa studio na maktaba ukiendelea chuoni Habari
Maalum, Mkuu wa chuo bwana Jackson Kaluzi amesema tangu ujenzi ulipoanza mpaka
sasa wanaamini kuwa ujenzi utakamilika ndani ya miezi sita kama walivyo panga
kwani hadi sasa maendeleo ni mazuri.
Kaluzi amesema imani yao ni kubwa hasa juu ya mkandarasi
anayesimamia ujenzi huo kwani anaonyesha juhudi katika utendaji wake, ambapo
kila wiki na kila mwezi kuna hatua zinazotakiwa kufikiwa na matarajio yao yanaonekana kukamilika.
Aidha amesema pamoja na kuwepo na changamoto mbalimbali ikiwa
ni pamoja na jinsi ya kufikisha vifaa vya ujenzi katika eneo la ujenzi lakini
hayo yote yameshughulikiwa.
Kwa upande wake Injinia wa Elerai Constraction Company
Limited ni muda mfupi tangu waanze takribani mwezi mmoja lakini hadi sasa
wamefika hatua ya juu zaidi ya muda walioutumia.
Bwana Kimaro amezitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni
pamoja naukosekanaji wa maji maeneo ya karibu na kazi, hivyo hivyo inawagalimu
kufuata maji mbali, pia ardhi ina vumbi ambayo ni changamoto katika kazi,
lakini wanajitahidi kudhibiti kwa kumwaga maji mengi ardhini.
Injinia huyo amemaliza kwa kusema kuwa, kazi hii imekuwa na
faida kubwa kwa wakazi wanaoishi kuzuguka chuo cha Habari Maalum, kwani
wameweza kupata ajira.
No comments:
Post a Comment