Na Renalda Mwarabu
Mwalimu mlezi chuo cha Habari Maalum akizungumza na wasichana kwa habari ya nidhamu ya mavazi(Picha na Renalda Mwarabu). |
Mwalimu mlezi wa wanafunzi
ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha uongozi na usimamizi katika chuo cha
Habari Maalum, Ndugu Nestory Ihano, amewataka
wanafunzi wa kike chuoni hapo kuwa na nidhamu katika mambo mbalimbali
hasa suala zima la mavazi, kawani wamekuwa
wakienda kinyume na sheria za chuo kwa kuvaa mavazi yasiyo ya heshima.
Akizungumza na wasichana
mara baada ya kumaliza matangazo ya kila siku na kuomba kubaki na
wanafunzi wa kike kwa mazungumzo maalum, amesema wasichana wengi
wamejisahau katika suala la nidhamu ya mavazi, huku likiwa ni moja ya masuala nyeti katika
nidhamu chuoni hapo.
Bwana Ihano amesema
yeye hayuko tayari kuona mwanafunzi yeyote anavaa mavazi yasiyo ya heshima, na
kwamba endapo hali hiyo itaendelea
hakuto kuwa na msamaha wowote bali sheria kufuata mkondo wake.
Hali kadhalika amewataka wanafunzi wote ambao wamehama
kutoka katika mabweni ya chuo kutoendelea kulala katika mabweni hayo kwani wao
wamesha amua kuishi maisha yao ya kujitegemea
na kwamba chuo kinawatambua kama wanafunzi hivyo hawana haki ya kuendelea kuyatumia mabweni hayo.
Pamoja na kwamba wanafunzi wanao ishi katika mabweni ya chuo
wanaongozwa na sheria za namna ya kuishi, mlezi huyo amesema wanafunzi wamekuwa
wakienda kinyume na utaratibu na sheria za mahali hapo kwa kutokutoa taarifa
wanapotaka kufanya jambo lolote ama kwenda mahali popote na kujichukulia maamuzi yao binafsi .
Bwana Ihano amewataka pia kuonyesha hali ya utii na nidhamu
kwa watu wanao wazunguka ikiwa ni pamoja na walinzi wa mazingira ya chuo, kwani
kumekuwa na malalamiko kuwa wanafunzi wamekuwa wakibishana na walinzi pale
wanapohitajika kufuata sheria mbalimbali.
Aidha ametoa wito kwa wanafunzi hao wakike kuwa waangalifu
pindi wanapokuwa chuoni kwani kwani hali
ya kuto kutii inaweza kuwasababishia wao matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na
kujikosesha haki ya kuishi katika
mabweni ya chuo.
No comments:
Post a Comment