NA Elia Simon Gumbo
Mlezi wa wanafunzi katika chuo cha habari maalum Bwana Nestory
Ihano amehimiza uongozi wa chuo hicho kuwasilisha rasmi ratiba ya mazoezi kwa vitendo ambayo yamekuwa
yakiwasaidia wanafunzi kupata uzoefu wa
kazi wanazosomea katika kipindi cha muhula mpya wa mwaka 2016 .
Bwana Ihano akielezea umuhimu
wa ratiba hiyo ya mazoezi ya urushaji
vipindi amesema itasaidia wanafunzi masomo ya Uongozi na Uandishi wa Habari kuweza
kuutumia muda wao wa kimasomo vizuri kwa kujipatia ujuzi utakaoleta
mafanikio ya maisha yao ya chuoni na
baadae katika maeneo ya kazi.
Naye makamu mkuu wa taaluma
wa chuo cha Habari maalum bwana Lazarus Laizer ameeleza kuwa kuchelewa kidogo
kwa ratiba hiyo kumetokana na mabadiliko ya maboresho ya mtaala wa masomo ,
mabadiliko ya kiuongozi pamoja na maboresho ya vifaa.
Bwana Laizer amesema wataleta
mfumo mpya utakaowawezesha wanafunzi kuchagua aina ya vipindi wanavyotaka
kuviandaa ili kuleta ufanisi katika
maeneo yote ya mafunzo ikiwemo upande wa
magazeti ,redio na televisheni.
Naye waziri wa elimu katika
serikali ya wanafunzi ya chuo cha Habari maalum ndugu Albin Michavao,amethibitisha kupata
taarifa hizo za maboresho ya kitaaluma
na kuwataka wanafunzi wawe tayari kufanya kazi kwa ushirikiano na bidii kwani ndio msingi wa
mafanikio .
Mmoja wa wanafunzi wa habari
maalum Winifrida nicolaus ameeleza kufurahishwa
na mpango huo wa kuendelea kwa mazoezi
hayo kwani yamekuwa yakiwandaa wanafunzi kupata ujuzi na kuwaongezea uwezo wa
kujiamini wakiwa chuoni na hata nje ya chuo katika utendaji wa kazi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment