WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Thursday, 18 February 2016

WANAFUNZI CHUO CHA HABARI MAALUM WAASWA KUHESHIMU MATUMIZI YA MUDA

Na Renalda Mwarabu
                                     
                                     Mwalimu mlezi wa wanafunzi Bwana Nestory Ihano akizungumza na wanafunzi kwa habari ya kujali na kutunza muda. (Picha na Nickson Mafuru)

                                                 
Mwalimu mlezi wa wanafunzi ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha uongozi na usimamizi katika chuo cha Habari Maalum, ndugu Nestory Ihano, amewataka wanafunzi kuzingatia na kutunza matumizi ya muda, pindi wanapokuwa chuoni,                   hali ambayo itawapelekea kuwa watendaji wazuri baadaye.
Amesema hayo wakati akitoa matangazo ya kila siku katika chumba cha mikutano, mara baada ya kumaliza maombi ya asubuhi, na kusema kuwa tatizo la uchelewaji ni tatizo ambalo  linataka kuwa sugu kwa baadhi ya wanafunzi, na kwamba hali hiyo itapelekea maisha ya baadhi ya wanafunzi kuwa magumu siku za mbeleni  kwani muda ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo.
Bwana Ihano amewaasa wanafunzi kufuata sheria za chuo ikiwa ni pamoja na kujali muda wa vipindi, na kujifunza kufanya mambo kwa wakati husika, kwani baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakipuuzia kuhudhulia maombi ya asubuhi ambapo ni moja kati ya taratibu za chuo.
Naye mmoja wa waalimu wa chuo hicho, Mwalimu Emmy Kimaro, ambaye ni mwalimu wa masomo ya Public Relation and Advertising, Media Law, pamoja na somo la Studying techniques, amesema wanafunzi wanayo nidhamu, lakini ipo changamoto ya matumizi ya muda wa darasani, ambapo wanafunzi wamekuwa wakichelewa madarasani na kuwakuta waalimu wakiwepo tayari darasani, hali ambayo haitakiwi kitaaluma, kwani hupelekea  kupoteza umakini wa wanafunzi wanapokuwa madarasani.
                            
                                     Mwalimu Emmy Kimaro akizungumzia changamoto  zilizopo katika suala Zima la nidhamu ya muda chuoni Habari Maalum. (Picha na Asaph Bimila).

Mwalimu Emmy ameongeza kwa kusema kuwa, changamoto nyingine  inatokea pale ambapo wanafunzi wanaposhindwa kufika chuoni asubuhi kwa muda uliopangwa kwaajili ya maombi ya asubuhi .
Ametoa wito kwa wanafunzi wote kuwa, wanatakiwa kutumia muda walionao vizuri, kwani muda huwa haujirudii na kuhakikisha wanafanya kila jambo kwa wakati husika ili kufikia malengo yao.
Mmoja wa wanafunzi wa chuo cha Habari Maalum, Adelphina Pius, amezitaja baadhi ya sababu zinazompelekea mwanafunzi kutokuheshimu muda, kuwa ni pamoja na uvivu ,kuto kuutambua wajibu na malengo, lakini pia kutokujali umuhimu wa elimu,  na kupelekea wanafunzi kuto fanikiwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Kwa upande wake Makamo mkuu wa chuo taaluma, Bwana Lazarus Laizer, amesema nidhamu Ya utunzaji wa muda kwa wanafunzi, inaridhisha kwani amekuwa akifanya uchunguzi wa kina juu ya wanafunzi  na kuona kwamba wanafunzi wanajitahidi kujishughulisha katika nyanja mbalimbali za masomo muda wote wanapokuwepo chuoni.
 Lazarus amesema , siku za nyuma wanafunzi walikuwa wakizagaa hovyo na kuhakiki kuwa ni jambo la tofaauti sana, kuona kwamba katika muhula huu nidhamu ya matumizi ya muda imeimarika tofauti na siku za nyuma.
                    
                              Makamo Mkuu wa Chuo Taaluma Bwana Lazarus Laizer akizungumzia mwenendo wa              nidhamu ya muda kitaaluma chuoni Habari Maalum ( Picha na Asaph Bimila).

Aidha, Lazarus amesema bado kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wanafunzi, kwani wanachelewa kufika asubuhi katika muda wa maombi kwa kuzingatia kwamba, chuo kimejenga misingi yake juu ya maombi na hivyo kila mwafunzi anatakiwa kujihusisha katika suala zima la maombi lakini baadhi yao wamekuwa wakilipuuzia hilio.
Lazarus ametoa wito kwa wanafunzi wote kuwa wanatakiwa kufuata utamaduni wa chuo, kwani kila mahali kuna tamaduni na sheria ambazo ni lazima kila mtu aishi akiongozwa nazo.

No comments:

Post a Comment