Na Renalda Mwarabu
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Ban Ki Moon akitoa wasiwasi wake juu kuhusu mashambulizi ya kigaidi barani Afrika |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameelezea wasiwasi wake kuhusu
mashambulizi ya makundi ya kigaidi huko Burkina Faso, magharibi mwa
Afrika na kuitaka dunia isimame kukabiliana na hatari ya kuenea misimamo
mikali barani Afrika.
Ban Ki moon amesema hayo huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso
na kuongeza kuwa, nchi za ukanda huo zinapaswa kushrikiana kukabiliana
na matatizo mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa kazi, ubaguzi na
kinga ya kutoshitakiwa baadhi ya watu.
Ban alianza ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Afrika siku ya
Jumatano kwa kuanzia nchini Burkina Faso ambako alilakiwa na Alpha
Barry, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.
Jana Alkhamisi alionana na Rais Roch Marc Christian Kaboré wa nchi
hiyo, kama ambavyo alitembelea pia kituo kimoja na kuwasaidia chakula
watoto wadogo na kituo kimoja cha watoto wenye maradhi ya Ukimwi.
Mbali na Burkina Faso, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepangiwa kutembelea pia nchi za Mauritania na Algeria.
Ziara ya Ban Ki moon inafanyika katika hali ambayo hivi karibuni
kulitokea mashambulio ya kigaidi katika mji mkuu wa Burkina Faso,
Ouagadougou na kupelekea kuuawa zaidi ya watu 30. Chanzo Radio Terhan
No comments:
Post a Comment