Na Renalda Mwarabu
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James
Wambura amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kuwahabarisha watanzania
vyema katika mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na katika
kipindi cha siku mia za kwanza za awamu ya tano ya utawala wa Mheshimiwa
Dr. John Joseph Pombe Magufuli.
Naibu
Waziri uyo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wadau wa Habari katika
tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications
Limited.
“Hakika mmeonesha uwezo mkubwa, weledi na ukomavu mkubwa wa kisiasa na uzalendo kwa nchi yetu”.Alisema Bi.Wambura.
Mhe.Wambura
pia alieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ina dhamira ya dhati kabisa
ya kushirikiana na wadau wote vikiwemo Vyombo vya Habari, ambapo pia
mchakato wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambao ulishasomwa kwa
mara ya kwanza bungeni bado Serikali inaendelea kupokea maoni ya wadau
mbalimbali juu ya namna bora ya kuboresha Muswada huo.
Naibu
Waziri uyo alikazia umuhimu wa upashaji habari na kusema ni jambo
muhimu sana katika nchi yetu na kwaiyo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo iko tayari kufanya kazi na wadau wote.
“Kama
Serikali hatuwezi kuwakwepa wadau na ndio maana hata utaratibu wetu wa
kushughulikia makosa kwenye Vyombo vya Habari umebadilika. Tumekuwa ni
walezi zaidi badala ya kuwa viranja. Tunashauriana zaidi kuliko kutoa
adhabu. Tunaelimisha zaidi kuliko kusubiliana”
Naibu
Waziri uyo pia ameupongeza uongozi mpya wa jukwaa la wahariri na
kuhaidi kuwapa ushirikiano wa karibu katika kutatua masuala mbalimbali
ya Habari.
Kwa
upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Magazeti ya Mwananchi
Bw.Francis Nanai ameipongeza serikali kwa kuweka jitihada zaidi katika
kuboresha mahusiano mazuri na vyombo vya Habari na pia kwa afrika
mashariki Tanzania iko katika nafasi nzuri ukilinganisha na wenzetu
katika suala la uhuru wa vyombo vya habari.
(Chanzo Mo bog)
No comments:
Post a Comment