Shirika la ndege la taifa ATCL limefungua milango ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosomea fani zote zinazohusiana na usafiri wa anga, ikiwa ni kuunga mkono jitahada za serikali za kukabiliana na uhaba wa wataalama katika fani mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu wa ATCL mhandisi Ladislaus Matindi wakati wa mkutano wa wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha Elimu ya Usafiri kwa njia ya anga kiitwacho ShenYang AeroSpace University cha nchini China ulioitishwa na taasisi inayotoa ushauri wa elimu za vyuo vya nje ya nchi.
Amewaomba wazazi kote nchini kushirikiana na shirika lake ili faida iweze kupatikana, hivyo endapo wataalamu wazawa watapatikana kwa wingi ni wazi kuwa mapato na faida vitakuwa vikizunguka.
Naye mkurugenzi mkuu wa Global Education Link, Abdul-Malik Mollel amewatahadharisha wazazi walioamua kuwapeleka vijana wao kusoma nje ya nchi, kuhusu ongezeko la vyuo visivyokuwa na sifa kote duniani.
Katika hatua nyingine, Chuo kikuu cha Elimu ya usafiri wa cha ShenYang kimelikabidhi shirika la ndege nchini ATCL hati ya gharama zote kitakazotoa kwa ajili ya elimu ya miaka mitatu kwa mwanafunzi atayeteuliwa na shirika hilo kwenda kusomea masuala ya usafiri wa anga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
|
|
No comments:
Post a Comment