Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa Libya ipo katika hatari ya kurejea katika mgogoro wa nchi nzima, akielezea kuhusu hali tete ya usalama mjini Tripoli na mapigano yanayoendelea katika maeneo ya mashariki yenye hazina ya mafuta na maeneo mengine.
Ametoa tahadhari hiyo katika ripoti aliyoitoa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na kuanza tena ongezeko la mapambano ya kijeshi pamoja na mkwamo wa kisiasa katika taifa hilo.
Aidha Guterres amesema wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, kwa hivi sasa halina tena udhibiti nchini Libya, lakini athari zake zimeendelea kushuhudiwa, limekuwa likihusishwa na mashambulizi kadhaa katika maeneo tofauti, na jumuiya ya kimataifa katika taifa hilo bado ni shabaha ya mashambulizi.
Kuondoshwa kwa mtawala wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi mwaka 2011 kumeiingiza Libya katika machafuko
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
|
|
No comments:
Post a Comment