Wataalamu wa Saikolojia kutoka Royal Society for Public Health wameutaja mtandao wa Instagram kuwa unaongoza kusababisha magonjwa ya akili na msongo wa mawazo kwa vijana ikifuatiwa na SnapChat, Facebook, Twitter na YouTube.
Kwa mujibu wa Wanasaikolojia hao, miongoni mwa athari zinazosababishwa na Instagram pamoja na kusababisha magonjwa ya akili kama vile Bipolar, msongo wa mawazo uliopitiliza, kutamani kujiua, kukosa kujiamini na kuwa mpweke tofauti na mitandao mingine.
Katika utafiti uliofanywa kwa kuwahusisha zaidi ya 1,500 wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 24, zaidi ya watu 1,300 walitajwa kuathirika zaidi na mtandao huo ukilinganisha na mitandao mingine huku miongoni mwa sababu zilizotajwa kuongoza kwake ni pamoja na kuwa sehemu ya watu kutukanana na kuonesha maisha ya juu ambayo si halisi.
Aidha, utafiti umeonesha pia kuwa YouTube ina athari ndogo zaidi tofauti na mitandao mingine baadhi wakiutaja kama sehemu wanayopata furaha kwa kuangalia video zinazofundisha mambo mbalimbali
No comments:
Post a Comment