Vijana kutoka vyuo mbalimbali Jijini Arusha wamekutana katika Semina ilikuwa na ujumbe wa Self awereness is more than money iliyotelewa na Mjasiriamali Bi Gracy Lyimo Pamoja na Ndugu Maxwell Chaila ambaye alifundisha kuhusu Self Employment can take your life into first class,Semina hiyo ilifanyika katika viunga vya Chuo cha Habari Maalum Jijini Arusha Mapema wiki iliyopita.
Na Diu Mwiko
Na Diu Mwiko
Bi Gracy Lyimo akielezea kuhusu jinsi gani mtu anaweza akajitambua mwenyewe..(Picha Na Nickson Mafuru) |
Aidha katika Semina hiyo Bi Gracy amewataka vijana hao kujitambua pamoja na kutambua malengo yao na kuyafanyia kazi.
Nae msemaji wa pili katika semina hiyo Ndugu Maxwell Chaila aliongelea suala la kujiajiri mwenyewe na kusema kuwa linaweza kukuweka katika daraja la juu(Self employment can take your life into first class).
Katika semina hiyo Ndugu Maxwell amewataka vijana kufikiria kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa hali ambayo itawafanya kuwa huru.
Akiwakaribisha wasemaji hao mkuu wa Chuo cha Habari Maalum Bwana Jackson Kaluzi amesema kuwa semina kama hizo ni jambo la msingi sana kwani linaenda sambamba na maono ya Chuo hicho kitu ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi pindi watakapo hitimu masomo yao.
Burudani pia hazikukosekana ,mmoja wa wanafunzi kutoka katika chuo cha Habari Maalum anaekwenda kwa jina la Depper akionesha kipaji chake cha kuimba wakati wa semina hiyo(Picha Na Nickson Mafuru) |
Baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya semina hiyo.(Picha na Nickson Mafuru) |
It was wonderful
ReplyDelete