Chuo cha Habari Maalum kinachotoa mafunzo ya Uandishi wa Habari pamoja na Uongozi na Usimamizi kilichopo Jijini Arusha kimejizolea umaarufu katika ukanda huu wa kaskazini kwa utoaji wake wa mafunzo ulioegemea zaidi katika vitendo.
Kutokana na sifa hiyo, Chuo hicho kimeweza kupata tuzo mbalimbali ikiwamo ile ya utoaji elimu bora kwa ukanda huu wa kaskazini katika maonyesho ya nane nane Mwaka 2015.
Chuo hiki kimekuwa kikitoa mafunzo katika ngazi ya Shahada na Stashahada na kimekuwa kikipokea pia wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi.
Na Diu Mwiko Renalda Mwarabu Mwanafunzi wa Stashahada katika fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano akiwa studio katika kusoma kwa vitendo.(Picha na Nickson Mafuru) |
Mazezi kwa Vitendo ni miongoni mwa sifa ambazo vyuo vingi nchini havina kutokana na uhaba wa vifaa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi,hali hiyo ni tofauti na chuo cha Habari Maalum ambapo kuna vifaa vya kutosha na mazingira rafiki kwa kujifunzia.
No comments:
Post a Comment