WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Wednesday 24 February 2016

WANAFUNZI WA KIKE CHUONI HABARI MAALUM WAASWA KUZINGATIA NIDHAMU YA MAVADHI



Na Renalda Mwarabu
Mwalimu mlezi chuo cha Habari Maalum akizungumza na wasichana kwa habari ya nidhamu ya mavazi(Picha na Renalda Mwarabu).
 
Mwalimu mlezi wa wanafunzi  ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha uongozi na usimamizi katika chuo cha Habari Maalum, Ndugu Nestory Ihano, amewataka  wanafunzi wa kike chuoni hapo kuwa na nidhamu katika mambo mbalimbali hasa suala zima la mavazi, kawani wamekuwa  wakienda kinyume na sheria za chuo kwa kuvaa mavazi yasiyo ya heshima.

Akizungumza na wasichana  mara baada ya kumaliza matangazo ya kila siku na kuomba kubaki na wanafunzi wa kike kwa mazungumzo maalum, amesema wasichana wengi wamejisahau  katika  suala la nidhamu ya mavazi, huku likiwa ni moja ya masuala nyeti katika nidhamu chuoni hapo.

 Bwana Ihano amesema yeye hayuko tayari kuona mwanafunzi yeyote anavaa mavazi yasiyo ya heshima, na kwamba endapo hali hiyo itaendelea  hakuto kuwa na msamaha wowote bali sheria kufuata mkondo wake.

Hali kadhalika amewataka wanafunzi wote ambao wamehama kutoka katika mabweni ya chuo kutoendelea kulala katika mabweni hayo kwani wao wamesha amua kuishi maisha yao ya kujitegemea  na kwamba chuo kinawatambua kama wanafunzi  hivyo hawana haki ya kuendelea  kuyatumia mabweni hayo.

Pamoja na kwamba wanafunzi wanao ishi katika mabweni ya chuo wanaongozwa na sheria za namna ya kuishi, mlezi huyo amesema wanafunzi wamekuwa wakienda kinyume na utaratibu na sheria za mahali hapo kwa kutokutoa taarifa wanapotaka kufanya jambo lolote ama kwenda mahali popote  na kujichukulia maamuzi yao binafsi .

Bwana Ihano amewataka pia kuonyesha hali ya utii na nidhamu kwa watu wanao wazunguka ikiwa ni pamoja na walinzi wa mazingira ya chuo, kwani kumekuwa na malalamiko kuwa wanafunzi wamekuwa wakibishana na walinzi pale wanapohitajika kufuata sheria mbalimbali.

Aidha ametoa wito kwa wanafunzi hao wakike kuwa waangalifu pindi wanapokuwa  chuoni kwani kwani hali ya kuto kutii inaweza kuwasababishia wao matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na kujikosesha haki ya  kuishi katika mabweni ya chuo.


No comments:

Post a Comment