WELCOME HMC

2 / 3
3 / 3
3 / 3
2 / 3
Caption Two
3 / 3
Caption Three

Tuesday 16 February 2016

MATEKA WA BOKO HARAM WAKOMBOLEWA NIGERIA

Na Renalda Mwarabu

Makumi ya watu waliokuwa wanashikiliwa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram, wamekombolewa nchini Nigeria.
















Mateka waliokombolewa kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Sani Othman, Msemaji wa jeshi la Nigeria ameyasema hayo kupitia ripoti maalumu juu ya mafanikio ya operesheni za jeshi la nchi hiyo na Cameroon na kuongeza kuwa, askari wa nchi hizo mbili wamefanikiwa kukomboa mateka 112 kutoka mikononi mwa kundi hilo kupitia operesheni za pamoja.

Othman amesema kuwa, miongoni mwa watu waliokombolewa katika operesheni hizo zilizofanyika katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, ni pamoja na wanaume wanane, wanawake 36 na watoto 68.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, operesheni za kuwakomboa watu hao zimezaa matunda kwa ushirikiano wa jeshi la nchi jirani ya Cameroon katika kupambana na wanachama wa kundi hilo la kigaidi la Boko Haram. 

Ameongeza kuwa, katika operesheni hizo afisa mmoja wa jeshi la Cameroon amejeruhiwa vibaya baada ya gari alilokuwa ndani yake kulipukiwa na bomu katika moja ya vijiji vya jimbo hilo la Borno.

Hadi sasa zaidi ya watu elfu 17 wameuawa katika mashambulio ya wanachama wa genge hilo lililotangaza uungaji wake mkono kwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. 

Inelezwa kuwa, hadi sasa mamia ya watu wakiwamo wanafunzi wa kike bado wanashikiliwa na wanachama wa Boko Haram nchini Nigeria.(Kutoka  mtandaoni).

No comments:

Post a Comment